Shamal (Kushoto) akimpongeza Moreno kwa kufunga bao la pili.
Liverpool, England.
LIVERPOOL imeendelea vyema na maandalizi yake tayari kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England baada ya Jumatano Usiku kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ndogo ya Huddersfield.
Mabao yaliyoipa Livepool ushindi huo safi yamefungwa katika vipindi tofauti vya mchezo.
Alianza Marko Grujic kufunga katika kipindi cha kwanza kabla ya Alberto Moreno kufunga kwa mkwaju wa penati mwishoni mwa kipindi cha pili.
Katika mchezo huo Kocha wa Liverpool Mjerumani,Jurgen Klopp,alilazimika kumchezesha kipa wa akiba,Shamal George,kama mshambuliaji baada ya Lucas Leiva kuumia na benchi kukiwa hakuna mbadala.
0 comments:
Post a Comment