Dar es Salaam,Tanzania.
MKUTANO MKUU wa Simba SC leo kwa kauli moja umeridhia mabadiliko ya katiba ili kuweza kuifanya klabu hiyo kongwe nchini kuingia katika mfumo mpya wa kikampuni ambao utatoa nafasi kwa Wanasimba kuuza na kununua hisa.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi - Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama wengi ilishuhudiwa Agenda namba tisa (9) ambayo ilihusu "Taarifa ya kamati ya Maboresho ya Mfumo wa Uendeshaji” ikitawala zaidi kati ya kumi (10) zilizojadiliwa hali iliyopelekea Rais wa klabu hiyo,Evans Aveva,kuutangazia umma kuwa kama wanataka Simba SC ikiingia kwenye mchakato wa kampuni, maoni yao yamesikilizwa na yanaanza kufanyiwa kazi mara moja.
Hii ina maana kwamba kupitia mabadiliko hayo ya katiba,Mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji "Mo",ambaye amepania kununua asilimia 51 ya hisa za Simba SC kwa bilioni 20 ana nafasi kubwa ya kutimiza lengo lake hilo.
0 comments:
Post a Comment