728x90 AdSpace

Thursday, July 28, 2016

GUARDIOLA NA MAN CITY YAKE WAICHAPA DORTMUND 6-5 ICC

Shenzhen,China.

KOCHA Pep Guardiola ameiongoza klabu yake mpya ya Manchester City kuichapa Borussia Dortmund kwa penati 6-5 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya International Champions Cup (ICC) ulioisha hivi punde katika uwanja wa Shenzhen Longgang,China.

Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada timu hizo kwenda sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida.

Sergio Aguero alianza kuifungia Manchester City bao la kuongoza dakika ya 79 kabla ya Christian Pulisic kuifunga Borussia Dortmund bao la kusawazisha dakika ya 96 na kupelekea mshindi atafutwe kwa changamoto ya mikwaju ya penati na ndipo Manchester City walipoibuka wababe kwa penati 6-5 baada mlinda mlango wake Angus Gunn kupangua penati ya Mikel Merino wa Borussia Dortmund.

VIKOSI

Man City: Caballero (Gunn) |
Adarabioyo, Otamendi (Maffeo),Kolarov (Angelino) | Navas (Silva),Fernandinho,Fernando (Toure (Sterling)), Clichy (Denayer) | Zinchenko (Aleix García), Delph (Agüero) | Iheanacho (Bony (Nolito))

Borussia Dortmund : Bürki | Ginter (Merino), Bartra (Larsen), Sokratis (Bender), Schmelzer (Passlack) | Rode (Castro), Sahin (Bumic) | Mor (Pulisic), Leitner, Dembele (Kagawa) |Ramos (Hober)

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: GUARDIOLA NA MAN CITY YAKE WAICHAPA DORTMUND 6-5 ICC Rating: 5 Reviewed By: Unknown