Mauritius
TIMU za taifa za vijana waliochini ya umri wa miaka 17 za Afrika Kusini na Malawi zimefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya michuano ya soka kwa nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao ya nusu fainali iliyochezwa jana Ijumaa dhidi ya Kenya na Namibia.
Timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini maarufu kama Amajimbos imeichapa Kenya iliyokuwa mgeni mwalikwa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-0.
Hicho ni kichapo cha pili kikubwa kwa Kenya katika michuano huyo kwani katika mchezo wake wa awali kabisa ilichapwa na Malawi kwa mabao 5-0.
Mabao ya Amajimbos yamefungwa na Mjabulise Mkhize 10',Luke Le Roux 30',Lina Mchilizeli 37' na Bonga Dladla 73'.
Hiyo ni
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa Ijumaa,Malawi imechomoza na ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Namibia baada ya sare ya mabao 1-1 ya Peter Banda 51' (Malawi) na Eldery Morgan 88' (Namibia)
Ratiba ya Finali na Mshindi wa Tatu:
Mshindi wa Tatu: Jumapili Julai 31,2016
Kenya v Malawi
Fainali:Jumapili Julai 31,2016
South Africa v Namibia
Takwimu Muhimu za Michuano Hiyo:
Michezo iliyochezwa: 14
Mabao yaliyofungwa: 44
Ushindi Mkubwa: Malawi 5 Kenya 0 (Kundi B,Julai 26)
Mabao mengi katika mchezo Mmoja: 5 – Malawi 5 Kenya 0 (Kundi B, Julai 26);Seychelles 1 Namibia 4
(Kundi A, Julai 27)
Wafungaji
Mabao 4- Peter Banda (Malawi), Abram Tjahikika (Namibia)
Mabao 3 – Eldery Morgan (Namibia), Nicholas Mulilo
(Zambia)
Mabao 2 – Franck Chizuze (Malawi), Damiano Kola
(Zambia), Luke le Roux (South Africa),
Linamandla Mchilizeli (South Africa) , Fabrizio Mosa (Madagascar), Kenneth Mukuria (Kenya), Siphamandla Ntuli (South Africa) ,George Nyimbili (Zambia)
Bao 1 – Raphael Banda (Malawi), Bonga Dladla (South Africa) , Neehal Hurdoyal (Mauritius),Mathiot Juninho (Seychelles), Rivaldo Laksman (Namibia), Francisco Madinga (Malawi), Mswati Mavuso (South Africa),Mjabulise Mkhize (South Africa) , Matteo Monple (Mauritius), James Monyane (South
Africa), Kunda Nkandu (Zambia), Benjamin Phiri (Zambia), Tyreese Pillay (South Africa) ,Mwiza Siwale (Zambia)
0 comments:
Post a Comment