728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 24, 2016

    CAF YAPATA UDHAMINI MPYA TOKA TOTAL

    Cairo,Misri.


    Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.

    Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.

    Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.

    Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.

    Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon.

    Thamani ya mkataba huo haijawekwa wazi.

    Total itakuwa mdhamini mkuu wa:

    * Kombe la Taifa Bingwa Afrika
    * Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
    * Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
    * Super Cup ya Afrika
    * Kombe la Shirikisho
    * Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
    * Kombe la Futsal Afrika
    * Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23 Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji
    wa chini ya miaka 20
    * Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YAPATA UDHAMINI MPYA TOKA TOTAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top