728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 27, 2016

    NYOTA MWINGINE WA LIVERPOOL AJIUNGA NA AFC BOURNEMOUTH

    Bournemouth,England.

    MLINZI wa kimataifa wa Australia,Brad Smith,amejiunga na AFC Bournemouth akitokea Liverpool kwa ada ya £3m.

    Smith,22,amesaini mkataba wa miaka minne na anakuwa mchezaji wa pili kutoka Liverpool kujiunga na AFC Bournemouth baada ya Jordan Ibe aliyejiunga na klabu hiyo maarufu kama Cherries mwanzoni mwa mwezi huu kwa ada ya £6m.

    Smith amejiunga na AFC Bournemouth baada ya kushinda kupata nafasi katika kikosi cha kwanza Liverpool.Msimu uliopita Smith alifanikiwa kuichezea Liverpool jumla ya michezo minne ya ligi kuu.

    Mpaka sasa AFC Bournemouth imeshafanikiwa kusajili jumla ya wachezaji sita ambao ni Jordon Ibe, Nathan Ake, Lewis Cook, Lys Mousset na Emerson Hyndman.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA MWINGINE WA LIVERPOOL AJIUNGA NA AFC BOURNEMOUTH Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top