728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 25, 2016

    ICC:PSG BILA IBRAHIMOVIC BADO MOTO YAICHAPA INTER 3-1 MAREKANI

    Los Angels,Marekani.

    Paris-Saint Germain imeonyesha bado moto licha ya kuondokea na aliyekuwa nahodha na mshambuliaji wake mahiri,Zlatan Ibrahimovic,baada ya Jumapili usiku kuichapa Inter Milan kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya International Champions Cup (ICC) uliochezwa katika uwanja wa Oregon's Autzen
    Stadium wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 24,000.

    Shujaa wa Paris-Saint Germain katika mchezo huo alikuwa mlinzi wa kimataifa wa Ivory Coast,Serge Aurier,aliyefunga mabao mawili dakika za 15 na 87.Bao jingine la Paris-Saint Germain limefungwa na mlinzi wa kushoto wa Ufaransa,Layvin Kurzawa,dakika ya 61 kwa mkwaju wa faulo.

    Bao la kufutia machozi la Inter Milan limefungwa dakika ya 45 na mshambuliaji Stevan Jovetic kwa mkwaju wa penati uliotolewa baada ya Lucas Moura wa Paris-Saint Germain kuunawa mpira ndani ya boksi.

    VIKOSI

    Inter: Handanovic (Carrizo 71); D'Ambrosio,Miranda, Ranocchia, Erkin (Santon 71);Biabiany, Melo, Kondogbia (Zonta 76),Nagatomo (Bakayoko 71); Palacio, Jovetic

    PSG: Areola (Trapp 46); Aurier, Thiago Silva (Meunier 71), Kimpembe, Maxwell (Kurzawa 46); Stambouli (Georgen 83), Rabiot (Pastore 74); Lucas (Di Maria 83), Ben Arfa (Cavani 74), Ikone (Nkunku 74); Callegari

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ICC:PSG BILA IBRAHIMOVIC BADO MOTO YAICHAPA INTER 3-1 MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top