Glasgow, Scotland.
MLINZI Mkongwe wa Ivory Coast,Kolo Toure,amejiunga na Klabu ya Celtic ya Scotland kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Toure,35,amejiunga na Celtic baada ya kutemwa na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Liverpool aliyojiunga nayo mwaka 2013 akitokea Manchester City.
Akiwa na Liverpool Toure alifanikiwa kucheza michezo 71 na kufunga bao moja.Kabla ya hapo aliichezea Arsenal kwa miaka saba kisha Manchester City kwa miaka minne.Akifanikiwa kushinda mataji mawili ya ligi kuu England na matatu ya FA Cup.
0 comments:
Post a Comment