London,England.
BAADA ya kumkosa Gonzalo Higuain aliyejiunga na Juventus huku pia ikionekana kutishwa na bei ya mshambuliaji wa Lyon,Alexander Lacazette, klabu ya Arsenal imeripotiwa kuhamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Toulouse ya Ufaransa,Wissam Ben Yedder (Benyebut) mwenye thamani ya £8m.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinadai tayari Arsenal imeshafanya mkutano wa siri na wawakilishi wa Yedder,25, ambaye msimu uliopita alifanikiwa kuifungia Toulouse jumla ya mabao 23.
Wakati huohuo taarifa nyingine kutoka nchini Ufaransa zinadai kuwa Arsenal inapaswa kupambana kiume ili kumnasa mkali huyo wa mabao kwani klabu ya Sevilla ya Hispania nayo imeripotiwa kumuwinda nyota huyo kufuatia kutokuwa na uhakika wa kumbakisha mshambuliaji wake nyota Mfaransa,Kevin Gameiro,anayewindwa kwa nguvu zote na vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid.
Katika kipindi cha misimu minne alichoichezea Toulouse,Yedder,mwenye asili ya Tunisia,amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 70 idadi ambayo imevukwa na washambuliaji wawili pekee nchini Ufaransa ambao ni Zlatan Ibrahimovic na Alexandre Lacazette.
VIDEO!!
0 comments:
Post a Comment