728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 29, 2016

    KIRAFIKI:SIMBA SC YATEMBEZA KICHAPO KINGINE MOROGORO JIONI YA LEO,MASHABIKI WAMUIMBA MO

    Morogoro,Tanzania.

    SIMBA SC imeendelea vyema na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Moro Kids katika mchezo mkali wa kirafiki uliochezwa katika viwanja vya chuo cha Biblia kilichopo Bingwa,Morogoro.

    Ibrahim Ajib alianza kuifungia Simba SC bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kupokea pasi murua toka kwa Shiza Kichuya na kufanya Simba SC iende mapumziko ikiongoza kwa bao hilo moja.

    Kipindi cha pili Simba SC ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Ibrahim Ajib,Jamal Mnyate na kuwaingiza Mohamed Ibrahim na Danny Lwanga.Mabadiliko hayo yaliiongezea Simba SC kasi na uelewano na hatimaye kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wake mrefu Danny Lyanga.

    Lyanga alifunga bao hilo baada ya kumegewa pande safi na kiungo mpya wa klabu hiyo Mohammed Ibrahim toka wingi ya kushoto na kufanya Simba SC itoke uwanjani ikiwa na mtaji huo wa mabao mawili dhidi ya Moro Kids iliyokuwa imeundwa na vijana wadogo wanaochezea vilabu vya madaraja ya chini hapa mjini Morogoro.

    Kesho Jumamosi raha nyingine itahamia katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa (Morogoro) ambapo Mtibwa Sugar itashuka dimbani kuvaana na Mbeya City katika mchezo mwingine wa kirafiki ambao utakuwa hauna kiingilio.

    Mashabiki wataka Mohammed Dewji "MO"

    Mashabiki wa Morogoro nao wametaka mfadhili wa zamani wa klabu hiyo, Mohammed Dewji "MO",apewe timu ili Simba SC irejee katika dhama zake za kutwaa mataji.

    Soka Extra ambayo ilikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo wa leo ilishuhudia mashabiki wa Simba SC kila mara wakisimama,wakipiga makofi na kuimba Mo apewe timu tumeshoka kuitwa wa Matopeni.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIRAFIKI:SIMBA SC YATEMBEZA KICHAPO KINGINE MOROGORO JIONI YA LEO,MASHABIKI WAMUIMBA MO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top