California,Marekani.
ARSENAL imeitambia Kombaini ya Marekani ( MLS All Stars) baada ya kuichapa kwa jumla ya mabao 2-1 Katika Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa Alfajiri ya leo katika Uwanja wa Avaya ulioko huko San Jose,California.
Ikiwa bila ya nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza Arsenal ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 11 baada ya Joel Campbell kufunga kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya boksi na Laurent Ciman wa MLS All Stars.
Dakika ya 45 Mshambuliaji wa Ivory Coast,Didier Drigba,aliisawazishia MLS All Stars bao na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.Bao hilo limemfanya Drogba aifunge Arsenal mabao 16 katika michezo 16 aliyocheza dhidi ya klabu hiyo ya London.
Mchezo ukiwa unaelekea kuisha,Chuba Akpom,aliifungia Arsenal bao la ushindi dakika ya 87 akiunganisha krosi ya beki wa kushoto,Nacho Monreal,aliyepanda kusaidia mashambulizi.
VIKOSI
MLS-All Star XI:
Andre Blake (HT, David Bingham),Keegan Rosenberry (HT, Andrew Farrell ), Laurent Ciman (HT, Kendall Waston ), Jelle Van Damme (HT, Steve Birnbaum), Kellyn Acosta (57th Brandon Vincent ), Andrea Pirlo (32nd, Sacha Kljestan, 73rd, Clint Dempsey ), Kyle Beckerman (HT,Darlington Nagbe), Giovani dos Santos (HT, Wil Trapp ), Kaka (HT,Mauro Diaz), David Villa (33rd,Ignacio Piatti , 73rd, Chris Wondolowski ) , Didier Drogba (HT,Sebastian Giovinco, 76th, Cyle Larin)
Arsenal XI:
Petr Cech (67th, Emiliano Martinez),Kieren Gibbs (51st, Nacho Monreal),Krystian Bielk (51st, Calum Chambers), Rob Holding, Mathieu Debuchy (HT, Hector Bellerin),Mohamed Elneny (67th Gedion Zelalem) , Francis Coquelin (HT,Granit Xhaka), Alex Oxlade-Chamberlain, Jack Wilshere (HT, Alex Iwobi), Joel Campbell (68th, Jeff Reine Adelaide), Theo Walcott (67th Chuba Akpom)
0 comments:
Post a Comment