728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 21, 2016

    WAARABU KUZICHEZESHA YANGA v MEDEAMA MARUDIANO

    Cairo,Misri.

    SHIRIKISHO la soka Afrika,CAF,limewateua waamuzi kutoka nchini Morocco kuchezesha mchezo wa marudiano wa kundi A wa michuano ya shirikisho kati ya Yanga na Medeama FC.

    Katika mchezo huo utakaochezwa siku ya Jumanne Julai 26 katika uwanja wa Essipong Sports ulioko katika mji wa Sekondi-Takoradi,mwamuzi wa kati atakuwa Rédouane Jiyed mwenye umri wa miaka 36 ambaye atakuwa akisaidiana na waamuzi wasaidizi,Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou wote kutoka Morocco.

    Ikiwa Yanga itapoteza mchezo huo ama kutoka sare rasmi itakuwa imepoteza matumaini ya kutinga hatua ya nusu faini kwani haitakuwa na uwezo wa kuzifikia timu mbili za juu.

    Katika mchezo Wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

    Mbali ya mchezo huo mchezo mwingine wa kundi hilo utachezwa huko Lubumbashi,TP Mazembe watakuwa wenyeji wa MO Bejaia ya Algeria.

    Katika mchezo wa kwanza uliochezwa siku ya Jumapili huko Bejaia,Algeria timu hizo ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bila kufungana.

    TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa imejikusanyia pointi saba.Mo Bejaia ni ya pili ikiwa na pointi tano,Medeama FC ni ya tatu ikiwa na pointi mbili.Yanga inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAARABU KUZICHEZESHA YANGA v MEDEAMA MARUDIANO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top