Barcelona,Hispania.
KLABU ya Barcelona imeendelea kukiimarisha kikosi chake tayari kwa Msimu Mpya wa Ligi ya La Liga na Michuano Mingine hii ni baada ya Alhamis Usiku kutangaza kufanikiwa kuinasa saini ya Kiungo Mahiri wa Ureno na Valencia,Andre Gomes,kwa ada ya uhamisho ya €55m.
Gomes,22,ambaye awali alionekana kama angejiunga na Real Madrid kwa ada ya €65m kabla ya Barcelona kuingilia kati na Kumnyakua,amekubali mkataba wa Miaka Mitano na mapema wiki ijayo atatambulishwa mbele ya Mashabiki na Waandishi wa Habari wa Jimbo la Catalunya.
Akiwa na Valencia,Gomes, alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 78 na Kufanikiwa kupachika jumla ya mabao tisa tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Mestalla mwaka 2014-15 akitokea Benfica ya Nyumbani kwao Ureno.Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mwezi huu nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment