Liverpool,England.
Liverpool imetangaza kumsajili kwa uhamisho huru kipa wa zamani wa Arsenal,Muaustria Alex Manninger.
Manninger,39,amesaini mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufuzu majaribio yaliyodumu kwa muda wa zaidi ya wiki moja.
Kabla ya kutua Liverpool,Manninger,aliwahi kuvichezea vilabu vya Arsenal (1997-2002), Fiorentina, Espanyol,Udinese,Juventus na Augsburg iliyomtema mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuitumikia kwa miaka minne.
0 comments:
Post a Comment