728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 30, 2016

    AZAM FC YATOA WATATU KWA MKOPO,WAWILI SIMBA SC,MMOJA NDANDA FC

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame,Azam FC, wametangaza kuwatoa kwa mkopo nyota wake watatu kwenda Vilabu vya Simba SC na Ndanda FC.

    Nyota hao ni Mlinda Mlango Mwadini Ally Mwadini na Washambuliaji Ame Ally "Zungu" na Joseph Kimwaga.

    Mwadini Ally Mwadini na Mshambuliaji Ame Ally "Zungu" watakuwa na Simba SC katika msimu ujao wa ligi kuu huku Mshambuliaji Joseph Kimwaga ambaye msimu uliopita aliichezea Simba SC kwa mkopo akipelekwa Ndanda FC ya Mtwara

    Azam FC imeamua kuwatoa kwa mkopo nyota hao ili kuokoa viwango vyao hasa baada ya msimu uliopita kushindwa kupata nafasi katika vikosi vyake vya kwanza.Sababu nyingine ni kutoa nafasi kwa klabu hiyo kujipanga upya katika kipindi hiki cha usajili.

    Wakati huohuo,Azam FC,imetangaza kufanikiwa kumnasa Winga na Mshambuliaji wa Medeama ya Ghana,Enock Atta Agyjaye,kwa kandarasi ya miaka miwili.

    Agyjaye,18,ambaye alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Yanga katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa kundi A wa kombe la shirikisho ulioisha kwa sare ya bao 1-1 anatarajiwa kuwasili nchini leo Jumamosi akitokea nyumbani kwao Ghana tayari kuanza kazi ya kuitumikia Azam FC katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na ile ya Azam Confederation Cup maarufu kama FA Cup.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM FC YATOA WATATU KWA MKOPO,WAWILI SIMBA SC,MMOJA NDANDA FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top