728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 25, 2016

    WAKENYA WAMWAGA PESA KUIDHAMINI HULL CITY

    Hull, England.

    Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya imetia saini mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City ya Uingereza.

    Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull City kwa misimu mitatu.

    Wimbi la uchezaji kamari lavuma Kenya Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi ya Premia msimu utakaoanza mwezi ujao.

    Hull City watafungua msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya mabingwa Leicester City.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo,udhamini wa SportPesa ndio wa juu zaidi kuwahi kupokelewa na klabu hiyo katika historia yake ya miaka 112.

    Hull City imekuwa ikidhaminiwa na kituo cha burudani cha Flamingo Land.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAKENYA WAMWAGA PESA KUIDHAMINI HULL CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top