728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 26, 2016

    YANGA HOI SHIRIKISHO YACHAPWA 3-1 NA MEDEAMA

    Sekondi,Ghana.

    YANGA SC imepoteza matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Medeama SC katika mchezo mkali wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Sekondi-Takoradi,Ghana.

    Mabao ya Medeama SC katika mchezo wa leo yamefungwa na Mohammed Abass aliyefunga mara mbili dakika za 22 na 37 pamoja na Daniel Amoah aliyefunga bao moja dakika ya 3.

    Bao la kufutia machozi kwa upande wa Yanga limefungwa kwa mkwaju wa penati na winga,Simon Msuva.Mkwaju huo wa penati ulipatikana baada ya mshambuliaji Obrey Chirwa kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la boksi.

    Kwa matokeo hayo Medeama SC imefikisha pointi tano sawa na Mo Bejaia iliyo katika nafasi ya pili.Yanga imebaki mkiani na pointi yake moja baada ya kushuka dimbani mara nne.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA HOI SHIRIKISHO YACHAPWA 3-1 NA MEDEAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top