728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 21, 2016

    ARSENAL YAIZIDI UJANJA MAN UNITED NA KUMNASA NAHODHA WA NORWAY

    London,England.

    ARSENAL imeizidi ujanja Manchester United na kufanikiwa kumnasa Nahodha na beki mahiri wa kati wa timu ya taifa ya vijana ya Norway ya U16,Erik Tobias Sandberg,kutoka klabu ya Lillestrom SK.

    Habari kutoka Mtandao wa The Sun,zinasema Maskauti wa Arsenal walivutiwa na beki huyo baada ya mwezi Februari kumshuhudia akichezea Norway katika mchezo wa kimataifa dhidi ya England na kuamua kufanya kweli kuipata saini yake wakiwazidi ujanja wenzao wa Manchester United ambao nao walivutiwa na beki huyo.

    Sandberg mwenye uwezo mzuri wa kuusoma mchezo na kuzuia washambuliaji wasumbufu wasilete balaa langoni kwake amefanikiwa kukichezea kikosi cha vijana cha Norway jumla ya michezo minane na kufanikiwa kufunga bao moja.

    Kwa kuanzia Arsenal imempa Sandberg ufadhili ya masomo (scholarship) kabla ya mwezi Februari kumpa mkataba kwani atakuwa amefikisha umri wa miaka 17 ambao unatambulika kisheria katika duru za usajili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAIZIDI UJANJA MAN UNITED NA KUMNASA NAHODHA WA NORWAY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top