728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 07, 2015

    KIMENUKA:HIVI NDIYO UCHAWI UNAVYOTUMIKA KATIKA SOKA LA EPL,WAGANGA WA KIENYEJI WAPIGA PESA NDEFU

    Uchawi?Upo!!Baada ya mshambuliaji Emanuel Adebayor kumsahambulia mama yake mzazi kuwa anamroga na kumfanya ashindwe kuonyesha cheche zake dimbani,nyota mwingine wa Afrika Brown Ideye aliyekuwa akiichezea West Bromwich kabla ya kutimkia Ugiriki amedai kuwa wachezaji wengi wa ligi kuu England wanatumia uchawi ili wapate kuwa juu.
    Brown Ideye celebrates after scoring the first goal
                                                                   Brown Ideye

    Ideye amesema "Nawajua wachezaji wanaojihusisha na uchawi na hawawezi kujikwamua kwani huo ni mtego.Hawawezi kwa kuwa waganga wao ni watu wenye nguvu na ushawishi mwingi.Wanafanikiwa lakini mafanikio yao huwa ni ya muda mfupi sana huku wakipoteza pesa nyingi na majuto juu.

    Ideye ameongeza "Kama uchawi ungekuwa na msaada basi Messi na Ronaldo wasingekuwa kutwaa tuzo za wachezaji bora kila mwaka na badala yake zingetua mikononi mwa wachezaji wa Kiafrika.Nawashauri wachezaji wenzangu kuachana kabisa na mambo hayo kwani yanawapotezea muda na pesa nyingi.


    Mganga raia wa Benin aitwaye Marabout Degla amesema wachezaji hupewa dawa ambapo moja kati ya masharti yake huwa ni kutofanya mapenzi kwa siku tisa huku usiku wakilala huku wakiwa wamejifunika shuka jeupe pekee.

    Degla ameongeza kuwa wachezaji hupewa pete ambayo huwasaidia kuwatawala wachezaji wenzao na wapinzani pindi wawapo mchezoni.

    The Sun nalo limeongeza kuwa kuna mganga mmoja alifika hotelini ambako timu moja ya England ilipokuwa imeweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya na kutaka apewe £50,000 ili aisaidie klabu hiyo ifanye vizuri katika michuano hiyo hiyo ambapo wachezaji wa Kifrika waliopo katika timu hiyo walitaka mganga huyo apewe pesa hiyo lakini nahodha wa klabu alikataa katukatu na mpango huo kufa hapo hapo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIMENUKA:HIVI NDIYO UCHAWI UNAVYOTUMIKA KATIKA SOKA LA EPL,WAGANGA WA KIENYEJI WAPIGA PESA NDEFU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top