728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 26, 2015

    KOCHA LIVERPOOL ANA SIKU KUMI TU ZA KUOKOA KIBARUA CHAKE

    Meneja wa klabu ya soka ya Liverpool Brendan Rodgers atakua na siku kumi ngumu za kibarua chake katika timu hiyo, hayo yamesemwa na mlinzi wa zamani wa timu hiyo Mark Lawrenson.

    Liverpool ilipata ushindi wa matuta wa 3-2 dhidi ya klabu ya daraja la pili ya Carslisle baada ya kuishia na sare ya 1-1.

    Liverpool itakutana na Aston Villa na kisha Everton katika michezo inayofuata ya ligi kuu England.
    Lawrenson amesema kuwa Rodgers ''yupo katika hatari kubwa'' na timu hiyo imekosa hamasa.

    Akizungumza na BBC, ameongeza kuwa ''Sipendelei kuona waalimu wa vilabu wakifukuzwa mara kwa mara kwa sababu najua ni miongoni mwa kazi ngumu ila sio kwa michezo sita zaidi ya ushindi wa matuta ulioipata dhidi ya klabu ya daraja la pili''

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA LIVERPOOL ANA SIKU KUMI TU ZA KUOKOA KIBARUA CHAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top