728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 16, 2015

    TUMECHOKA:MASHABIKI ARSENAL WATAKA WILSHERE APIGWE BEI HARAKA

    London,England.

    Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki wa Arsenal wameitaka klabu yao hiyo kumuuza mara moja kiungo wao kipenzi Jack Wilshere,23.

    Mashabiki hao wamefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na majeruhi ya mara kwa mara yanayoendelea kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa England na kusisitiza kuwa Arsenal inapaswa kufanya haraka kwani Wilshere amekuwa hana msaada klabuni kwasababu muda mwingi amekuwa akikaa nje ya dimba akiuguza majeraha yasiyokwisha.

    Kauli hii ya mashabiki wa Arsenal imekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Arsenal kutangaza kuwa Wilshere ambaye alitarajiwa kurejea dimbani wikendi iliyopita atakuwa nje ya dimba mpaka krismasi kutokana na kuhitaji upasuaji mwingine wa kuondoa kabisa tatizo la majeruhi linalomkabili.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TUMECHOKA:MASHABIKI ARSENAL WATAKA WILSHERE APIGWE BEI HARAKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top