
Simba haijawahi kuifunga Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani tangu timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa ilipopanda daraja na zaidi Wekundu hao wamekwishaambulia sare moja na kufungwa mechi mbili.
Katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo, Kocha wa Simba, Mwingereza Dylan Kerr, ameonekana kutaka wachezaji wake kupiga pasi 100 bila kupoteza kwa adui.
Katika mazoezi yao yaliyofanyika juzi asubuhi kwenye Uwanja wa Disuza, Kerr alitumia muda mwingi kutaka wachezaji wake kupiga pasi nyingi zinazofika ili waweze kuibuka na ushindi.
(Kwa habari kamili usikose kujipatia nakala yako ya Gazeti la DIMBA Leo)
0 comments:
Post a Comment