728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 15, 2015

    IMERUDI TENA:FAHAMU HISTORI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA,KISHA TUAMBIE NI SEHEMU IPI IMEKUMBAMBA ZAIDI


    Wakati michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo jumanne usiku sokaextra.blogspot.com imeona ni vyema ikuletee mambo kadhaa ya kufahamu kuhusu michuano hii mikubwa na tajiri zaidi katika ngazi ya vilabu duniani.

    Ili kurahisisha ujumbe/habari hii ieleweke vizuri sokaextra.blogspot.com imekuja na mtindo wa swali na jibu

    Je,michuano hii ilianza lini?

    Kwa mara ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa ilianza kutimua vumbi lake mwaka 1955–56 ambapo jumla ya vilabu 16 vilishiriki.Vilabu hivyo ni AC Milan (Italy),AGF Aarhus (Denmark), Anderlecht (Ubelgiji), DjurgÃ¥rden (Sweden), Gwardia Warszawa (Poland), Hibernian (Scotland),Partizan (Yugoslavia), PSV Eindhoven (Uholanzi), Rapid Wien (Austria), Real Madrid (Spain), Rot-Weiss Essen (Ujerumani Magharibi), Saarbrücken (Saar ), Servette (Uswisi), Sporting CP (Ureno), Stade de Reims (Ufaransa), and Vörös Lobogó (Hungary).

    Je,timu ipi imeutwaa ubingwa huu mara nyingi zaidi?

    Real Madrid ndiyo timu iliyoutwaa ubingwa huu mara nyingi zaidi ikiwe imeutwaa mara 10.

    Mchezo wa kwanza wa michuano ulichezwa lini/kati ya timu zipi?

    Mchezo wa kwanza kabisa wa ligi ya mabingwa wa Ulaya ulipigwa Septemba 4,1955 na matokeo kuwa sare ya goli 3–3 kati ya Sporting CP na Partizan. 

    Goli la kwanza la michuano lilifungwa na nani?

    Goli la kwanza la michuano hiyo lilifungwa na João Baptista Martins wa Sporting CP.Huku fainali za kwanza zikipigwa Parc des Princes,Ufaransa kati ya Stade de Reims na Real Madrid.Mpaka mwisho Real Madrid 4-3 Reims.Magoli ya washindi yalifungwa na Alfredo Di Stéfano,Marquitos huku Héctor Rial akifunga mara mbili.

    Je,wimbo wa michuano ulitungwa lini/uliimbwa na nani?

    Wimbo huo maarufu sana ulitungwa na mtunzi Tony Britten mwaka 1992 baada ya kuombwa kufanya hivyo na UEFA.Katika kuunogesha wimbo huo Britten aliwashirikisha London's Royal Philharmonic Orchestra na sauti zinazosikika katika wimbo huo ni kutoka Academy ya St. Martin.Kiitikio cha wimbo huo kina jumla ya lugha tatu ambazo ni lugha rasmi za UEFA, Kiingereza,Kijerumani na Kifaransa.Wimbo huo una urefu wa dakika tatu.

    Kikombe/Ubingwa

    Kila mwaka timu bingwa huzawadiwa kikombe ambacho k 1967.Ikiwa timu yoyote itafanikiwa kukitwaa kikombe hiki mara tatu mfululizo au mara tano katika nyakati tofauti basi hupewa jumla kiwe mali yake.

    Je ni timu ngapi zimefanikiwa kutwaa kikombe hicho moja kwa moja?

    Timu sita pekee ndiyo zimepata heshima hiyo.Timu hizo ni Real Madrid, Ajax, Bayern Munich, Milan, Liverpool na Barcelona.

    Je,kikombe hicho kina uzito kiasi gani?

    Kikombe hicho chenye urefu wa 74 cm kina uzito wa 11 kg.Kilibuniwa na sonara maarufu Jörg Stadelmann wa Bern Uswisi baada ya kile cha awali kutolewa kama zawadi kwa Real Madrid mwaka 1966 baada ya timu hiyo ya Hispania kukitwaa kikombe hicho kwa mara ya sita.

    Je,kikombe hicho kiligharimu pesa kiasi gani kukitengeneza?

    Kikombe hiki kiligharimu kiasi cha francs 10,000 tu za Kiswisi.

    Waamuzi:Mwamuzi wa michuano hii hapaswa kuvuka umri wa miaka 45 hata awe mahiri kiasi gani akifikisha umri huo inabidi akae pembeni na wengine waingie

    Medali:Tangu 2012–13 jumla ya medali 40 za dhahabu zimekuwa zikitolewa kwa bingwa wa michuano hiyo huku nyingine 40 za fedha zikitolewa kwa mshindi wa pili.

    Zawadi ya Pesa

    UEFA inatoa €2 kwa washindi wa mtoano na €3 kwa timu itakayokuwa imetolewa.Kwa kutinga hatua ya makundi pekee UEFA huzipa timu kiasi cha €12m. 

    Mchanganuo kamili uko kama ifuatavyo...

    Hatua ya kwanza kufuzu: €200,000
    Hatua ya pili kufuzu: €300,000
    Hatua ya tatu kufuzu: €400,000
    Kushindwa kuvuka mtoano: €3,000,000
    Washindi hatua ya mtoano: €2,000,000

    Malipo/zawadi hatua ya makundi: €12,000,000

    Ushindi hatua ya makundi: €1,500,000,Sare hatua ya makundi: €500,000,Hatua ya 16 bora: €5,500,000,Robo fainali: €6,000,000,Nusu fainali: €7,000,000,Mshindi wa pili: €10,500,000,Bingwa wa michuano hukpmba jumla ya €15,000,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IMERUDI TENA:FAHAMU HISTORI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA,KISHA TUAMBIE NI SEHEMU IPI IMEKUMBAMBA ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top