Hawthorns, West Brom
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994,Everton imetoka nyuma na kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu nchini England.
Everton iliyokuwa mgeni wa West Bromwich Albion katika mchezo pekee wa ligi kuu hapo jana jumatatu ilijikuta ikiwa nyuma kwa magoli mawili ya Saido Berahino na Craig Dawson kabla ya kuamka na kupata magoli matatu kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mawili na kisha kutengeneza jingine lililofungwa na Arouna Kone.
Historia ya mwaka 1994 yarudiwa.
Mara ya mwisho Everton kutoka nyuma na kushinda mchezo wa ligi kuu ilikuwa ni mwaka 1994 pale ilipoibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Wimbledon na kukwepa mkasi wa kushuka daraja baada ya kuwa nyuma katika kipindi kirefu cha mchezo.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo.....
WEST BROM (4-2-3-1): Myhill; Dawson, Evans, Olsson (Chester 28), Brunt; Fletcher, Yacob (Lambert 85); McClean, Morrison, Berahino; Rondon (Gardner 69).
EVERTON (4-1-4-1): Howard; Browning (Gibson 72), Jagielka, Funes Mori, Galloway; Barry; Deulofeu, McCarthy, Barkley, Naismith (Kone 72); Lukaku (Lennon 89
0 comments:
Post a Comment