Barcelona,Hispania.
Lionel Messi anafahamika kwa umahiri wake wa kusakata kandanda lakini linapokuja suala la kupiga mikwaju ya penati kidogo amekuwa akipata wakati mgumu sana kufunga akiwa ndani ya eneo la miguu 12 ya mtu mzima,amekuwa akikosa sana.
Katika penati 10 alizapiga hivi karibuni Messi amekosa jumla ya penati 4 huku ya karibuni ikiwa ni ile dhidi ya Levante wikendi iliyopita.
Ifuatayo ni rekodi ya Messi katika upigaji wa penati akiwa na FC Barcelona
Messi amekosa jumla ya penati 13 kati ya 61alizopiga akiwa na jezi ya FC Barcelona katika ligi ya La Liga na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyekosa penati nyingi zaidi katika kipindi cha muongo mmoja katika ligi ya Hispania.Pia Messi amekosa jumla ya penati 3 kati ya 11alizopiga katika michuano ya klabu bingwa Ulaya na hivyo kufikisha jumla ya 16 katika michezo 72 akiwa na FC Barcelona ambayo ni sawa na 20% huku mpinzani wake Cristiano Ronaldo yeye akionekana kuwa juu kwani amekosa 10% pekee katika penati zote alizopiga mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment