728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 22, 2015

    FA YAWATIA HATIANI COSTA,GABRIEL,YAJIANDAA KUWALIMA ADHABU KUBWA

    London,England.

    Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya Arsenal jumamosi iliyopita.

    Mshambuliaji huyo alimfanyia madhambi pamoja na kumchapa vibao mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny katika dakika ya 43 ya mechi.Mchezaji huyo ana hadi saa kumi na mbili hapo alhamisi jioni kujibu mashtaka hayo.

    Naye Beki wa Arsenal Gabriel Paulista ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu kwa tabia yake wakati alipopewa kadi nyekundu huku Santi Carzola akionywa kuhusu tabia yake mbaya.

    Wakati huohuo vilabu vyote viwili vimeshtakiwa kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake chini ya sheria za FA.

    Vilabu vyote viwili pamoja na Gabriel vina hadi saa kumi na mbili jioni siku ya alhamisi kujibu mashtaka hayo.

    Kufuatia sakata hilo Costa na Gabriel huenda wakafungiwa michezo mitatu mitatu kila mmoja.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FA YAWATIA HATIANI COSTA,GABRIEL,YAJIANDAA KUWALIMA ADHABU KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top