Manchester,England.
Unaweza kusema vyovyote vile unavyojisikia lakini maamuzi ya shirikisho la vilabu vya soka barani Ulaya (UEFA) hayawezi kubadilika.
Taarifa kutoka England zinasema klabu ya Manchester United imelijia juu shirikisho la vilabu vya soka barani Ulaya UEFA kwa kitendo chake cha kumpa tuzo mchezaji ya mchezaji bora wa mechi mlinzi wa PSV Endhoven Hector Moreno ambaye alimchezea rafu na kumvunja mara mbili mlinzi wake wa kushoto Luke Shaw katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa jumanne iliyopita.
Manchester United imeponda vikali uteuzi huwa kwa madai kuwa mtu aliyefanya unyama kwa mwinzie kiasi kile hakupaswa kupewa tuzo yenye heshima kama ile.
Moreno alimrukia na kumvunja mifupa miwili ya mguu wa kulia Luke Shaw dakika ya 16 ya mchezo huo ulioisha kwa Manchester United kulala kwa goli 2-1.Luke Shaw atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita akiuguza jeraha hilo
0 comments:
Post a Comment