Winga wa Manchester United Mdachi Memphis Depay ametoa kauli ambayo pengine kila mpenda mpira duniani anaweza asiifurahie kabisa na kuhisi huenda nyota huyo ni mgonjwa.
Depay ambaye leo jumanne atarejea tena katika dimba la Phillips lakini safari hii akiwa na Manchester United kuivaa klabu iliyomlea ya PSV Eindhoven ya Uholanzi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya amesema ikiwa ataifunga klabu yake ya zamani ya PSV basi atashangilia kama ambayo angeshangilia pindi ambapo angeifunga klabu yoyote ile duniani.
Akifanya mahojiano kuelekea mchezo wa leo usiku,Depay,21 amesema "Watu wengi wameniuliza kama nitashangilia ikiwa nitafunga goli,naiheshimu PSV lakini nitashangilia.Mpira ni game (mchezo) na kufunga ni kitu spesho hivyo lazima nitashangilia tu".
Depay alijiunga na Manchester United msimu huu akitokea PSV kwa ada ya £25m ambako aliibuka mfungaji bora akiwa na magoli 22 na kuipa taji la Eredivisie klabu hiyo kongwe ya Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment