Arsenal imekumbana na kipigo cha bao 2-1 toka kwa Dynamo Zagreb katika mchezo wa kundi F wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya katika dimba la Stadion Maksimir mjini Zagreb.
Arsenal ilijikuta nyuma dakika ya 24 baada ya winga Alex Oxlade Chamberlain kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Josip Pivaric huku goli la pili la Zagreb likifungwa dakika ya 54 na Junior Fernandez kwa kichwa safi akiunganisha kona ya El Arabi Hilal Soudani.
Mabadiliko ya kumuingiza Theo Walcott yalizaa matunda baada ya nyota huyo kuifungia Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 79 akiiwahi pasi safi ya Alexis Sanchez.
Giroud aendelea kumvua nguo Arsene Wenger..
Mshambuliaji Olivier Giroud ameendelea kuonyesha kuwa yeye siyo mtu sahihi wa kuibeba Arsenal baada ya kucheza madhambi ya makusudi na kulimwa kadi nyekundi na kukifanya kikosi cha Arsenal kicheze pungufu katika vipindi vyote viwili.
Giroud alipewa kadi ya pili ya njano baada ya kumkwatua kwa makusudi nyota wa Zagreb Ivo Pinto.
0 comments:
Post a Comment