BURUDANI.Mwamuzi mmoja wa soka nchini Brazil ameingia matatani baada ya kuonyesha kitako cha bunduki aina ya bastola kama ishara ya kujilinda dhidi ya wachezaji waliokuwa wakimshushia kipigo uwanjani kufuatia kutoridhishwa na maamuzi yake.
Mwamuzi huyo Gabriel Murta ambaye pia ni ofisa wa polisi alilazimika kuikumbuka bastola yake iliyokuwa kiunoni baada ya kupigwa teke kisha ngumi na wachezaji wa klabu ya Belo wakati akichezesha mechi ya soka ya daraja la chini nje kidogo ya jiji la Belo Horizonte.
Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha soka cha eneo hilo Giuliano Bozzano amesema Mutra atatafutiwa mwanasaikolojia ili amuweke sawa kiakili baada ya tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment