728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 11, 2016

    LA LIGA:BARCELONA YAGONGWA NYUMBANI NA KITIMU KILICHOPANDA DARAJA (+VIDEO)

    Barcelona, Hispania.

    FC BARCELONA imetolewa nishai nyumbani kwake Nou Camp baada ya Jumamosi Usiku kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Derpotivo Alaves.

    Katika mchezo huo ulioshuhudiwa FC Barcelona ikianza huku nyota wake wa ushambuliaji Lionel Messi na Luis Suarez wakiwa benchi ilijikuta nyuma baada ya dakika ya 39 Deyverson kuifungia Alaves bao la kuongoza akiunganisha krosi ya Kiko Femenia.


                                                 

    Jeremy Mathieu aliisawazishia FC Barcelona dakika za 47 ya kipindi cha pili lakini bao hilo halikuiokoa miamba hiyo ya Catalunya kwani Ibai Gomez aliipa tena uongozi Alaves baada ya kufunga bao dakika ya 64 na kufanya mchezo uishe kwa wenyeji FC Barcelona kulala kwa mabao 2-1.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LA LIGA:BARCELONA YAGONGWA NYUMBANI NA KITIMU KILICHOPANDA DARAJA (+VIDEO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top