728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 27, 2016

    SIMBA SC LAZIMA WAKAE - PLUIJM


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema inauma kupoteza mchezo dhidi ya Stand United lakini inabidi kuyaacha nyuma matokeo hayo kwa sababu hayawezi kubadilika tena.

    Yanga ilipata kipigo cha kwanza msimu huu cha bao 1-0 katika mchezo dhidi ya Stand United uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Akizungumza jana Pluijm alisema matokeo hayo wameyaacha na sasa wanaelekeza nguvu zao katika michezo inayofuata ili kubadili matokeo yaliyo mazuri ukiwemo dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki hii.

    “Hatuna furaha kwa matokeo tuliyoyapata dhidi ya Stand United,inatubidi tujiandae vizuri kubadili matokeo yetu yajayo,”alisema.

    Akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Simba Pluijm alisema kama wanahitaji kucheza michuano ya kimataifa ni lazima wapate matokeo mazuri.

    Alisema anaiheshimu Simba lakini hana hofu nayo, kwani ni lazima timu hiyo ikae chini kwa kuwa wanajipanga kuchukua pointi tatu.

    Kocha Pluijm alisema

    wanachotakiwa kufanya ni wachezaji kucheza kwa kujiamini na ukakamavu jambo ambalo amekuwa akilisisitiza kwa wachezaji wake mara kwa mara sio tu katika mchezo huo bali michezo yote.

    Kikosi cha Yanga kimeweka kambi Pemba kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.

    Mechi hiyo ni muhimu kwa timu zote kwani Yanga itahitaji ushindi ili kurudi kwenye mstari katika mbio za kutetea taji lake huku Simba ikihitaji ushindi ili kujiweka sawa katika kuwania taji la kwanza baada ya miaka minne.

    Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 10 huku Simba ikiongoza kwa pointi 16 na Stand United ikishika nafasi ya pili kwa pointi 12.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC LAZIMA WAKAE - PLUIJM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top