Jinja,Uganda.
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Kilimanjaro Queens, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Cecafa wa wanawake baada ya jioni hii kuifunga Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa jioni ya leo huko Jinja.
Mpaka mapumziko Kilimanjaro Queens ilikuwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Mshambuliaji wake hatari Mwanahamisi Omari dakika za 24 na 45.
Bao la Kenya limefungwa dakika ya 64 na Christine Nafula.Kilimanjaro Queens imekuwa bingwa wa pili wa michuano hiyo baada ya ndugu zao Zanzibar kuutwaa ubingwa huo mwaka 1986.
0 comments:
Post a Comment