Fanja,Oman.
KIUNGO wa Kimataifa wa Tanzania,Mrisho Khalifan Ngasa (Pichani) akitambulishwa baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Klabu ya Fanja inayoshiriki ligi kuu ya nchini Oman.
Ngasa aliyewahi kutamba na vilabu vya Yanga,Simba,Azam FC,Kagera Sugar na Toto Africans ya Mwanza pamoja na Free State Stars ya Afrika anakuwa mchezaji wa pili kutoka Tanzania kujiunga na klabu hiyo baada ya Danny Lyanga aliyejiunga na klabu hiyo jana Jumanne.
0 comments:
Post a Comment