Canaria,Hispania..
REAL Madrid imeshindwa kupata ushindi kwa mara ya pili mfululizo katika kipindi kisichozidi wiki moja baada ya Jumamosi Usiku kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Las Palmas katika mchezo mkali na mgumu wa ligi ya La Liga uliochezwa katika uwanja wa Gran Canaria.
Real Madrid ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Marco Asensio.Bao hilo halikudumu sana kwani dakika tano baadae yaani dakika ya 38 Tana Taunausú aliifungia Las Palmas bao la kusawazisha na kufanya timu hizo ziende sare zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili walikuwa ni Real Madrid tena waliotangulia kuandika bao la pili dakika ya 67 kupitia kwa mtokea benchi Karim Benzema aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi ya Marco Asensio.
Mchezo ukiwa umebakisha dakika tano kumalizika Araujo aliifungia Las Palmas bao la kusawazisha dakika ya 85 na kuinyima Real Madrid kupata ushindi katika mchezo wa pili mfululizo.
0 comments:
Post a Comment