London,Uingereza.
MWANARIADHA nyota wa Uingereza na mshindi mara nne wa medali za dhahabu za Olimpiki,Mohamed Muktar Jama Fara,maarufukamma Mo Farah amesema anatamani siku moja kuja kuwa kocha/mtaalamu wa mazoezi ya viungo (Fitness Coach) wa klabu ya Arsenal.
Pichani:Mo Farah akifanya mazoezi na kikosi cha Arsenal.
Farah,33,mwenye asili ya Somalia na ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo yenye makao yake makuu katika uwanja wa Emirates aliambia jarida la The Sunday Times Magazine kwamba yuko tayari kufanya Kazi na klabu hiyo siku za usoni.
Amesema "Kitu kimoja ninachokipenda sana ni mpira (soka) na nina mahusiano mazuri na Arsenal.
Nilianza kuishabikia Arsenal mara ya kwanza nilipofika hapa Uingereza wakati huo nikiwa mtoto sana.Nilipenda walivyokuwa wakicheza.Pia nilivutiwa nao kwa kuwa walikuwa na wachezaji wengi wenye asili ya Afrika.
Siki moja ningependa kupata nafasi ya kufanya kazi Arsenal,kama kocha wa mazoezi ya viungo.Mimi ni muumini mkubwa wa namna mwili unavyoweza kufanya makubwa ikiwa utapatiwa mazoezi stahiki.Alimaliza Farah.
Kwa sasa Tony Colbe ndiye kocha/mtaalamu wa mazoezi ya viungo wa Arsenal na alianza jukumu hilo mwaka 1998.Msaidizi wake ni Craig Gant.
0 comments:
Post a Comment