Swansea,Wales.
Gael Clichy (Pichani) akipongezwa na Kelechi Iheanacho na wachezaji wenzake wa Manchester City baada ya kuifungia timu hiyo bao la kwanza Uwanja wa Liberty katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Swansea City kwenye mchezo wa Kombe la Ligi England usiku huu.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na Clichy dakika ya 49 na Aleix Garcia Serrano dakika ya 67, wakati la Swansea City lilifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 93.
Aidha katika mchezo huo nahodha wa Manchester City,Vincent Kompany,aliyekuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi alikutana na balaa jingine baada ya kuumia tena katika mchezo wake wa kwanza baada ya miezi mitano ya matibabu.
0 comments:
Post a Comment