Dortmund, Ujerumani.
WACHEZAJI wa Borussia Dortmund (Pichani) wakipongezana baada ya jana Ijumaa Usiku kuichapa Freiburg kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo mkali wa ligi ya Bundesliga uliochezwa katika uwanja wa Signal Park Iduna.
Mabao ya Borussia Dortmund katika mchezo huo yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang 45', Lukasz Piszczek 53' na Raphael Guerreiro 90'. Bao la kufutia machozi kwa Freiburg limefungwa na Maximilian Philipp 60'.
Ushindi huo umeifanya Borussia Dortmund iwe imeshinda michezo yake minne kati ya mitano ya Bundesliga msimu huu huku ikiweka rekodi ya kucheza michezo 24 nyumbani bila kupoteza.
Sasa Borussia Dortmund imechupa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga baada ya kufikisha alama 12 sawa na Bayern Munich ambayo leo itashuka dimbani kucheza na Hamburg SV.
0 comments:
Post a Comment