London, Uingereza.
USIOMBE kusifiwa,tena na mtu anayejua kusifia,mbona utajuta na Usipokuwa makini unaweza ukavimba kichwa ukajiona tayari uko juu ya dunia.
STAA wa Arsenal,Mesut Ozil,amekoshwa vilivyo na kiwango cha kinda wa klabu hiyo Alex Iwobi na kusema kuwa aina ya soka la kijana huyo Mnigeria ni mchanganyiko wa ufundi na radha za mastaa aliowahusudu sana zamani ,Jay-Jay Okocha na Mdachi Edgar Davids.
Akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Arsenal’s matchday programme,Ozil,amesema “Nikimtazama Alex anavyocheza ananikumbusha mjomba wake Jay-Jay Okocha.Alikuwa ni mchezaji niliyependa kumtazama.Amesema
"Alex ana ufundi na radha ya mchanganyiko wa Jay-Jay Okocha na Edgar Davids.Ni makini na imara anapokuwa na mpira,mzuri kwenye kujilinda na hatari mbele ya lango la wapinzani.
“Anaendelea vizuri sana na kama atacheza kwa kiwango hiki hiki kwa msimu wote,atafika mbali.
Msimu huu Iwobi,20,ambaye ni mpwa wa staa wa zamani wa Nigeria,Jay Jay Okocha, ameichezea Arsenal michezo mitano pia ametajwa katika orodha ya wachezaji 40 wanaowania tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka 2016 wa Ulaya maarufu kama European Golden Boy Award.
0 comments:
Post a Comment