Manchester, Uingereza.
PAUL Pogba (Pichani) akipiga kichwa kufunga bao lililoiwezesha Manchester United kuichapa Leceister City mabao 4-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa mchana wa leo katika uwanja wa Old Trafford,Manchester.
Mpaka mapumziko Manchester United ilikuwa mbele kwa mabao hayo manne yaliyofungwa na Smalling, Juan Mata pamoja na Marcus Rashford.
Bao la kufutia machozi kwa Leceister City limefungwa Kipindi cha pili na Gray kwa mkwaju mkali wa mbali baada ya kumzidi maarifa Jesse Lingaard.
Ushindi huo umeifanya Manchester United kuchupa mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 12.
0 comments:
Post a Comment