728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 21, 2016

    HII HAPA KAULI YA SERIKALI BAADA YA SIMBA SC KUTAKA MECHI ZAKE ZICHEZWE UWANJA WA TAIFA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WAZIRI wa Habari Vijana,Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba Serikali haina pingamizi kwa Simba kurejesha mechi zake Uwanja wa Taifa kutoka wa Uhuru, Dar es Salaam.

    Nape amesema kwamba wenye mamlaka ya kurejesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzaniz za Simba Uwanja wa Taifa ni Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

     “Sisi hatuna tatizo,wao wamalizane na Bodi ya Ligi na TFF,”alisema

    Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya wiki hii Simba SC kuomba kurejesha mechi zake za Ligi Kuu Uwanja wa Taifa kutoka wa Uhuru, baada ya kubaini Uwanja wa Uhuru haupo vizuri.

    Katibu wa Simba SC,Patrick Kahemele alisema juzi mjini Dar es Salaam kwamba wachezaji wao watatu waliumia katika mchezo uliopita wakishinda 1-0 dhidi ya Azam FC Jumamosi kutokana na ubaya wa eneo la kuchezel la Uwanja wa Uhuru.

    “Vile vipira vya kwenye nyasi bandia pale uwanjani vimeharibika kutokana na kutotumika kwa muda mrefu, kwani vimepigwa jua, vimefubaa na kuwa

    kama vipande vya chupa,hivyo kuhatarisha usalama wa wachezaji wanapoanguka,”alisema Kahemele.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII HAPA KAULI YA SERIKALI BAADA YA SIMBA SC KUTAKA MECHI ZAKE ZICHEZWE UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top