728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 30, 2016

    YANGA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU KUHUSU JEZI ZAKE MPYA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Uongozi wa Yanga unapenda kuwatangazia wanachama,mashabiki na wapenzi kuwa klabu bado haijatoa jezi rasmi za kuvaliwa na wapenzi wake zenye nembo ya mdhamini mpya wa Yanga.

    Kuna taarifa za uwepo wa jezi feki mitaani zenye nembo ya Yanga pamoja na mdhamini mkuu tunatoa TAHADHARI kwa wapenzi wa Yanga kutonunua jezi hizo mana zinatengenezwa kwa Lengo la kuhujumu mapato ya klabu.

    Tumeshatoa taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo jeshi la polisi na endapo mtu atakutwa amevaa hiyo jezi atawajibikia kuisaidia polisi katika uchunguzi.

    Klabu itatoa taarifa sahihi ya lini jezi zake rasmi zitaanza kuwa mitaani.

    Epuka kununua kisicho halali cha Yanga. .Epuka kuvaa jezi feki yenye jina la QUALITY GROUP.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU KUHUSU JEZI ZAKE MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top