MARIO Balotelli ameendelea kuonyesha kuwa alifeli Liverpool kwa bahati mbaya tu na si kwamba kiwango kilikwisha,hii ni baada ya usiku huu kuifungia OGC Nice bao moja ambalo hata hivyo halikuweza kuinusuru na kichapo cha mabao 5-2 toka kwa FK Krasnodar katika mchezo mkali wa kundi I wa michuano ya Europa Ligi uliocheza katika uwanja wa Kuban Stadium.
Bao hilo alilolifunga kwa mkwaju mkali wa mbali katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza limemfanya Balotelli awe ameifungia OGC Nice mabao matano katika michezo minne iliyopita.
FK Krasnodar ilipata mabao yake kupitia kwa Fedor Smolov (22),Joaozinho (33, 65 pen) pamoja na Ari (86, 90+3).Mabao ya OGC Nice yamefungwa na Mario Balotelli (42) pamoja na Wylan Cyprien (71).
0 comments:
Post a Comment