728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 27, 2016

    DONDOO MUHIMU KUELEKEA PAMBANO LA BORUSSIA DORTMUND v REAL MADRID


    Westfalenstadion,Ujerumani.

    MACHO na Masikio ya wapenda kabumbu wengi duniani leo hii yataelekezwa Westfalenstadion ambapo miamba wa Hispania,Real Madrid ( Los Merengues ),watakuwa ugenini Signal Iduna Park kuvaana na watukutu Borussia Dortmund katika mchezo wa kundi F wa hatua ya pili wa michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.

    Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa utavuta na kusumbua hisia za wapenda kabumbu wengi ,Soka Extra kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya kimataifa imeona ni vyema ikakuletee dondoo muhimu za mchezo huo utakaoanza saa 3:45 Usiku.

    Kabla ya mchezo wa leo Borussia Dortmund na Real Madrid wamekutana mara sita katika misimu mitano iliyopita ya ligi ya mabingwa Ulaya.Mara mbili katika hatua ya makundi,mara mbili robo fainali na mara mbili nusu fainali.

    Timu hizo zilikutana mara ya mwisho msimu wa 2013-14 katika hatua ya robo fainali na Real Madrid kufuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

    Katika mchezo wa awali uliochezwa Hispania,Real Madrid,ilishinda kwa mabao 3-0 kwa mabao ya Gareth Bale,Isco na Cristiano Ronaldo kabla ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa nchini Ujerumani kwa mabao ya Marco Reus.

    Aidha timu hizo zimekutana mara tano katika ardhi ya Ujerumani.Borussia Dortmund imeshinda mara tatu,Real Madrid haijashinda mchezo wowote.Zimetoka sare mara mbili.

    Nyumbani-Ujerumani.

    Ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Borussia Dortmund imeshinda michezo yake saba kati ya tisa ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.Imetoka sare mchezo mmoja,ikipoteza mmoja huku ikishindwa kupata bao katika mchezo mmoja pekee.Hii ikiwa ni Novemba 2013 pale ilipochapwa mabao 2-0 na Arsenal

    Ugenini-Ujerumani.

    Real Madrid hawajashinda mchezo wowote kati ya michezo yao mitano waliyocheza nyumbani kwa Borussia Dortmund.Wamefungwa michezo mitatu na kutoka sare mara mbili.

    Majeruhi/Wachezaji watakaokosekana:

    Borussia Dortmund:Durm (Goti),Reus (Nyonga)

    Real Madrid:Casemiro (Enka),Marcelo (Nyonga)

    Vikosi tarajiwa 





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DONDOO MUHIMU KUELEKEA PAMBANO LA BORUSSIA DORTMUND v REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top