Manchester,Uingereza.
MENEJA wa Leicester City Muitaliano,Claudio Ranieri,ameitaka Manchester United kuachana mara moja na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wake Mwingereza,Danny Drinkwater kwani staa huyo hauzwi.
Tamko hilo la Ranieri limekuja baada ya mapema wiki hii kuibuka kwa taarifa kuwa Manchester United inapanga kujaribu kumsajili Drinkwater ,26,aliyewahi kuwa kuwa sehemu ya kikosi chake cha vijana ili kuipa makali safu yake ya kiungo ambayo msimu huu imeonyesha kulega lega.
Akifanya mahojiano na gazeti la The Guardian, Ranieri,amekiri kuijua adhima hiyo ya Manchester United lakini amesisitiza kuwa kiungo huyo hauzwi kwa dau lolote lile na kuongeza kuwa Leceister City haiko tayari kuona nyota wake yoyote yule anaihama klabu hiyo hivi karibuni.
Ranieri amekumbusha kuwa Drinkwater hana kipengele cha mauzo (Clause) kwenye mkataba wake kama iliyokuwa kwa NG'olo Kante aliyehamia Chelsea hivyo hakuna namna ambayo itawapa mwanya Manchester United kumnyakua kirahisi.
0 comments:
Post a Comment