728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 24, 2016

    MAMELODI SUNDOWNS YAFUZU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


    Tshwane,Afrika Kusini.

    MAMELODI Sundowns ya Afrika Kusini imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya usiku huu kuichapa Zesco United ya Zambia kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili uliochezwa katika uwanja wa Lucas Moripe huko Tshwane.

    Mamelodi Sundowns ilianza kujipatia bao lake la kwanza dakika ya 5 tu ya mchezo kupitia kwa Anthony Laffor aliyefunga akimalizia kazi nzuri ya Keagan Dolly.

    Dakika ya 64 Percy Tau aliifungia Mamelodi Sundowns bao la pili kwa kichwa akiunganisha krosi ya Tebogo Langerman na kufanya mchezo uishe kwa mabao hayo mawili kwa bila.

    Ushindo huo umeifanya Mamelodi Sundowns ifuzu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa awali uliochezwa huko Ndola,Zambia wikendi iliyopita.

    Vikosi

    Mamelodi Sundowns: Onyango; Langerman,Nthethe, Arendse, Mbekile - Kekana -Mabunda (Soumahoro 88'), Tau (Modise 79') -Dolly, Billiat, Laffor

    ZESCO United: Banda; Oluwafemi, Bahn,Odhiambo,Silwimba - Ching'andu (Kambole 62'), Chaila, Chama, Mtonga (Mbombo 73') -Mwanza (Mwape 59'), Were


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAMELODI SUNDOWNS YAFUZU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top