Manchester,England.
SHIRIKISHO la soka barani Ulaya,UEFA,leo limetoa orodha ya wachezaji 40 watakaochuana kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 21 maarufu kama UEFA Golden Boy Award.
Katika orodha hiyo ligi kuu za England na Ujerumani zimeongoza kwa kutoa wachezaji wengi katika kinyang'anyiro hicho chenye hadhi kubwa zaidi Ulaya kwa wachezaji vijana.
Baadhi ya wachezaji wa ligi kuu ya England waliobahatika kupenya kwenye kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Marcus Rashford,Dele Alli na Alex Iwobi.Wengine ni Ruben Loftus-Cheek,Marko Grujic Kelechi Iheanacho na Leroy Sane.Ujerumani ni Julian Brandt Andreas Christensen Kingsley Coman na Mahmoud Dahoud.
Kingsley Coman
Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 2003 na gazeti la michezo ya Italia la Tuttosport na mwaka jana ilitwaliwa na mshambuliaji wa Manchester United,Anthony Martial.
Wachezaji wengine waliowahi kuitwaa tuzo hiyo huko nyuma ni pamoja na Lionel Messi,Sergio Aguero,Raheem Sterling na Paul Pogba.
Orodha Kamili:
Ubelgiji:Belgian Jupiler Pro league: Leon Bailey (Gent), Youri Tielemans (Anderlecht).
Ujerumani:Bundesliga: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Andreas Christensen (Borussia Monchengladbach), Kingsley Coman (Bayern Munich), Mahmoud Dahoud (Borussia Monchengladbach), Ousmane Dembele (Borussia Dortmund), Breel Embolo (Schalke), Alen Halilovic (Hamburg), Renato Sanches (Bayern Munich), Jonathan Tah (Bayer Leverkusen).
Croatia: Ante Coric (Dinamo Zagreb).
Uholanzi Eredivise: Riechedley Bazoer (Ajax), Nathan (Vitesse), Jairo Riedewald (Ajax)
Uingereza English Premier League: Leroy Sane (Manchester City), Dele Alli (Tottenham), Demarai Gray (Leicester), Marko Grujic (Liverpool), Kelechi Iheanacho (Manchester City), Alex Iwobi (Arsenal), Ruben Loftus Cheek (Chelsea), Marcus Rashford (Manchester United).
Ufaransa Ligue 1: Gabriel Boschilia (Monaco), Emmanuel Mammana (Lyon), Almamy Touré (Monaco).
Italia Serie A: Amadou Diawara (Napoli), Gianluigi Donnarumma (AC Milan), Gabriel Barbosa (Inter Milan), Olivier Ntcham (Genoa).
Ureno Portuguese Primeira Liga: Gonçalo Guedes (Benfica), Ruben Neves (Porto).
Urusi: Aleksandr Golovin (CSKA Moscow).
Scotland: Moussa Dembele (Celtic).
Hispania:La Liga: Marco Asensio (Real Madrid), Carlos Fernandez (Sevilla), Lucas Hernández (Athletic Bilbao), Tonny Sanabria (Real Betis).
Ukraine: Viktor Kovalenko (Shakhtar Donetsk)
0 comments:
Post a Comment