728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 22, 2016

    EMMANUEL ADEBAYOR ASHINDWA KUENDANA NA KAULI MBIU YA UKAWA


    Lyon,Ufaransa.

    UNAIKUMBUKA ile kauli mbiu ya UKAWA ya kipindi cha uchaguzi wa mwaka jana wa Rais,Wabunge na Madiwani.Ile iliyosema Ukawaaaaaa mabadilikoooooo,mabadiliko Ukawaaaaaaaaa!!.

    Basi kauli mbiu hiyo imeonekana kuwa kitendawili kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Togo,Emanuel Adebayor,kwani jamaa ameshindwa kabisa kubadilika.

    Ishu iko hivi Adebayor,31,ambaye kwa sasa hana timu tangu alipotemwa na Crystal Palace mwezi Juni mwaka huu alipata bahati ya kutakiwa na Lyon ya Ufaransa hivi karibuni.

    Taratibu zote muhimu zikafanyika na mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal,Manchester City na Tottenham akasafiri mpaka Lyon kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mwisho kabla hajasaini kuichezea Lyon.

    Lakini ghafla taarifa zikaibuka kuwa uhamisho huo umeshindikana baada ya mazungumzo kuvunjika katika dakika za mwisho kwa kile kilichodaiwa kuwa Lyon ilitaka kumsajili Adebayor kwa sharti kuwa hataruhusiwa kuichezea Togo katika fainali zijazo za AFCON na yeye akakataa.

    Baada ya taarifa hizo kuendea kusambaa kwa kasi kubwa mfano wa moto wa petroli kwenye nyasi kavu huku Lyon ikinyooshewa vidole vya chuki karibu kila pande za nchi ya Togo,Rais wa klabu hiyo Bruno Genesio,ameamua kuvunja ukimya na kufichua sababu iliyofanya klabu yake ishindwe kumsajili Adebayor. 

    Genesio amesema Lyon haikushindwa kumsajili Adebayor kwa madai kuwa alikataa kutoshiriki AFCON bali ilishindwa kwa sababu mchezaji huyo alikuwa akivuta sigara na kunywa pombe wakati akifanyiwa usaili [Interview].

    Amesema "Tulikuwa na nafasi katika kikosi chetu kwa ajili ya Adebayor.Kweli tulihitaji kumsajili.Nilipanga kukutana naye kwa ajili ya kahawa na mazungumzo hapa Lyon.Lakini cha kushangaza alipofika tu akaagiza whisky na kuichanganya kwenye kahawa yake.Huku akiwa amening'iniza sigara mdomoni mwake.

    Kilichoniijia mara ya kwanza kwenye akili yangu ni kuwa Adebayor hakuwa na nafasi kwenye klabu yetu hiyo nikaachana naye.Lyon haiwezi kuwa na mchezaji aina ya Adebayor.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EMMANUEL ADEBAYOR ASHINDWA KUENDANA NA KAULI MBIU YA UKAWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top