728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 22, 2016

    HUU NDIYO MUDA AMBAO DANGOTE ASEMA ATAIFANYA ARSENAL KUWA MALI YAKE


    New York,Marekani.

    Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.

    Dangote ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho mwaka uliopita.

    Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.

    ''Hakuna tatizo kwamba atakinunua klabu hicho'' na si tatizo la fedha ,alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .

    ''Pengine miaka mitatau au mine.Swala ni kwamba tunachangamoto nyingi.Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia swala la ununuzi huo.Sitaangalia biashara peke yake bali pia nitaibadili Arsenal kuwa timu ya vikombe.

    Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasi cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha

    simenti cha mjini Lagos.

    Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliyopo katika ligi kuu ya Uingereza.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUU NDIYO MUDA AMBAO DANGOTE ASEMA ATAIFANYA ARSENAL KUWA MALI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top