KLABU ya Valencia imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Pako Ayestaran ikiwa ni miezi sita tangu impe jukumu hilo.
Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Valencia imesema klabu imeamua kumtimua Ayestaran,53,kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu.
Mpaka sana Valencia imepoteza michezo yake yote minne ya msimu mpya wa ligi ya La Liga na inaburuza mkia katika msimamo wa ligi.
Ayestaran alipewa jukumu la kuinoa Valencia mwezi machi mwaka huu akichukua nafasi ya Muingereza,Gary Neville,ambaye naye alifutwa kazi kutokana na matokeo mabovu.
Wakati huohuo Valencia imemtangaza beki wake wa zamani Mhispania Vero Gonzalez kuwa kocha wake mpya wa muda.
Vero aliichezea Valencia zaidi ya michezo 200 kati ya mwaka 1984 na 1993.Pia amewahi kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo katika nyakati tatu tofauti huku mwaka 2008 akifanikiwa kuipa klabu hiyo ubingwa wa kombe la Copa del Rey.
0 comments:
Post a Comment